Tuesday, September 8, 2009

NINI MAANA YA ELIMU KWA TANZANIA??????

Nikawaida kwa watanzania kuwapeleka watoto wao shule wakifikisha umri wa miaka 4-7 kwaajili ya elimu ya nursary kuelekea shule ya msingi. hali inaongeza wa tanzania wengi kuwa wanaenda shule asubuhi na kurudi jioni? na wengine kugombania usafiri na adha nyingine nyingi kama hizo
swali langu kwenu watanzania ni nini maana ya Elimu kwetu?
Tunashuhudia maendeleo ya wazi kwa nchi za jirani kupitia elimu hiii, hali inayofanya tuwapeleke watoto wetu wakasome shule hizo,kwa kutumia gharama kubwa na tabu nyingi
tunafanya hayo yote iwaje, kwa faida gani?
Nishazoea kuona watu wenye elimu wakiongea kiingereza na lugha nyingine za kigeni hasa wakiwa mbele ya makundi ya watu,nashindwa kuelewa vzuri je kwetu watanzania elimu ni kuonge kiingereza kama ni ndio kiingerza je kuna haja gani ya kuwa tunafundishwa hizo lugha tuuu
Naipenda tanzaniasababu ni nchi yangu, ila mm ni binadamu nina wivu wa maendeleo nikiona nchi zingine, je elimu hii ambayo kila mzazi wa tanzania anajitahidi kumpa mwanaye ina manufaa kwa maisha yakee, au elimu kwetu nikuwa na lundo la vyeti visivo na manufaa kwetu?
let us talk